.
.
.

Adhabu ya FA dhidi ya wachezaji hawa waliotemeana mate uwanjani…


Pamoja na kukataa kwamba hakumtemea mate mshambuliaji wa New Castle Papis Cisse, beki wa Man United, Jonny Evans amefungiwa mechi sita na Shirikisho la soka England FA.

Naye Papis Cisse amefungiwa michezo saba na Shirikisho hilo.

FA imetoa adhabu hiyo baada uya kuthibitisha kupitia mkanda wa video hiyo katika mchezo uliochezwa jumatano iliyopita katika uwanja wa St. James Park ambapo Man U waliibuka na ushindi wa goli 1-0, goli lililofungwa na Ashley Young.



Adhabu hiyo itamfanya beki huyo kukosa mchezo wa robo fainali dhidi ya Arsenal siku ya jumatatu kwmenye uwanja wa Old Tranford na michezo mingine atakayoikosa ni ile dhidi ya Tottenham, Liverpool, Aston Villa, Manchester City, na Chelsea.

Kwa upande wa Cisse atakosa michezo dhidi ya Everton, Arsenal, Sunderland, Liverpool, Tottenham,Swansea na Leicester
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment